Hii ni baada ya wataalamu kugundua kuwa bangi ina hatari ndogo ya matumizi mabaya ikilinganishwa na dawa nyingine za kulevya kama heroni. Utafiti wa FDA (Food and Drug Administration) pia unaonyesha kuwa bangi ina kiwango cha chini cha kusababisha uzoefu kwa watumiaji wake. FDA ni shirika linalosimamiwa na Wizara ya Afya na Huduma kwa Binadamu nchini Amerika. Kwa sasa, bangi imo katika Kitengo cha Kwanza kama dawa yenye hatari kubwa ya matumizi mabaya na uwezo wa kusababisha watumiaji kushindwa kujitegemea kisaikolojia au kimwili. Watafiti wanapendekeza kuwekwa katika Kitengo cha Tatu, kilicho na uzoefu wa wastani hadi wa chini kimwili na kisaikolojia.

Shares
  • getufmradio
  • getufmradio

Share This

Share this post with your friends!

Share This

Share this post with your friends!