Kulingana na taarifa ya polisi, washukiwa hao walikamatwa katika eneo la Vonza kaunti ya Kitui, baada ya gari moja kuripotiwa kuibwa katika kaunti ya Machakos.
Ripoti inabaini kuwa waalifu hao wana rekodi za uhalifu na walishtakiwa awali katika mahakama moja ya Machakos kwa wizi wa kimabavu.
Aidha, uchunguzi huo pia umegundua kwamba washukiwa hao ni sehemu ya genge la majambazi ambalo hutekeleza uhalifu kati ya Nairobi, Mlolongo, Machakos, Makueni na kwenye mpaka wa Kenya na Tanzania, ambapo magari ya wizi huuzwa.
Kulingana na maafisa wa polisi, washukiwa hao hukodisha magari wakidai yanatumika katika sherehe za harusi au shughuli za kampuni, lakini hutoweka na magari hayo.
Kesi dhidi yao zinasubiri kusikizwa katika mahakama za Makueni na Machakos.
Recent Comments