Mbuzi takriban 170 waliobiwa juzi katika eneo la Kiamiramba walipatikana jioni ya kuamkia leo kwenye mbuga ya wanyama ya Meru National Park upande WA Isiolo.
Kulingana na wafugaji waliokuwa wakifuatilia, dege iliona mbuzi hawa mwendo wa saa kumi na mbili na kuelekea saa moja jioni.
Baadae, makabiliano makali yalizuka kati ya maafisa wa kitengo cha KWS wakisaidiana na askari wa Kituo cha Kiamiramba.
Ingawa hawakuweza kukamata jangili hata mmoja kwa sababu walikuwa wamejihami, walifanikiwa kupata mbuzi wote, lakini inasemekana walikuwa wamemchukua mmoja na kumla.
Kwa usaidizi wa kitengo cha KWS, mbuzi hawa walipelekwa kwenye kituo cha polisi cha Kina ambako wanapatikana sasa.

Recent Comments