Shares
  • getufmradio
  • getufmradio

Mwanamke kutoka Kithare Sublocation, eneo la Ganga, Tharaka nithi, amehukumiwa kifungo cha mwaka mmoja gerezani baada ya kuwakataza watoto wake kuhudhuria shule, akidai kuwa alisikia sauti ya Mungu ikimwamuru asiwapeleke hadi Mungu atakapozungumza tena.

Watoto hao wanatarajiwa kurejea shuleni wakati wowote kuanzia leo, kufuatia uamuzi wa mahakama.

Afisa msimamizi wa masuala ya watoto katika eneo bunge la Maara, Bw. Mawira, ameonya vikali wazazi na walezi wanaokiuka haki za watoto kwa misingi isiyo na msingi wa kisheria. Amehimiza jamii kushirikiana na mamlaka kuhakikisha kila mtoto anapata haki yake ya elimu kama ilivyoainishwa kikatiba.

Share This

Share this post with your friends!

Share This

Share this post with your friends!