Igembe Kusini, Meru – Mbunge wa Igembe Kusini, John Paul Mwirigi, amesisitiza umuhimu wa kufuata sheria na taratibu zinazohitajika katika utekelezaji wa mradi wa usambazaji wa umeme katika eneo hilo.
Akizungumza na Getu FM, Mwirigi alieleza kuwa usambazaji wa umeme ni moja ya miradi aliyopatia kipaumbele, akifichua kuwa hatua kubwa tayari zimepigwa ili kuhakikisha maeneo mengi yanaunganishwa na gridi ya taifa.
“Tunahakikisha kuwa miradi hii inatekelezwa kwa kufuata sheria zote husika. Nia yetu ni kuona kuwa kila mwananchi anapata huduma hii muhimu bila vikwazo,” alisema Mwirigi.
Mbunge huyo aliahidi kushughulikia changamoto zilizopo ili kuhakikisha kuwa mradi huo unakamilika kwa wakati, akisisitiza kuwa umeme ni kiungo muhimu kwa maendeleo ya uchumi na ustawi wa wakazi wa Igembe Kusini.
Recent Comments