Igembe South, Meru – Mbunge wa Igembe South, John Paul Mwirigi, ameweka wazi ajenda yake ya maendeleo, akisisitiza kuwa atazidi kusukuma miradi muhimu katika eneo hilo licha ya changamoto zilizopo.
Akizungumza na Getu fm Radio, Mwirigi alieleza kuwa moja ya miradi aliyopigia prioriteti ni usambazaji wa umeme kwa wakazi wa Igembe South. Alisema kuwa tayari hatua zimepigwa katika kuhakikisha kuwa maeneo mengi yanaunganishwa na gridi ya taifa, huku akiahidi kushughulikia changamoto zilizopo ili kukamilisha mradi huo.
“Tumeanzisha miradi mingi ya maendeleo, ikiwemo usambazaji wa umeme. Hii ni hatua kubwa kwa sababu umeme ni nguzo muhimu kwa maendeleo ya uchumi wa eneo letu,” alisema Mwirigi.
Mbunge huyo pia alizungumzia changamoto zinazokumba utekelezaji wa baadhi ya miradi lakini akaahidi kushirikiana na wadau wote kuhakikisha kuwa maendeleo yanatekelezwa kwa ufanisi kwa manufaa ya wananchi wa Igembe South.

Recent Comments