Hospitali ya Mediheal imekana madai yoyote ya makosa kufuatia ripoti ya uchunguzi iliyoibua tuhuma kwamba kituo hicho cha matibabu kilikuwa kitovu cha mtandao haramu wa ulanguzi wa viungo vya binadamu.
Wamiliki wa hospitali hiyo wametetea taratibu zake za upasuaji wa kupandikiza figo, wakitoa wito kwa mtu yeyote mwenye ushahidi wa kweli kwamba alikatwa kiungo bila idhini kujitokeza na kutoa ushahidi.
Wakizungumza na wanahabari siku ya Jumatano, Aprili 23, wawakilishi wa kisheria wa hospitali hiyo walisisitiza kuwa huduma zote za kitabibu zinazotolewa katika hospitali hiyo hufanywa kwa kufuata sheria na maadili ya kitaaluma, chini ya usimamizi wa wataalamu waliothibitishwa.
Hospitali hiyo iliingia katika vichwa vya habari vya kimataifa kufuatia uchunguzi wa pamoja wa vyombo vya habari vya Ujerumani—Deutsche Welle (DW), ZDF na Der Spiegel—ambao ulifichua mtandao wa kimataifa wa wafadhili na wapokeaji wa viungo unaoratibiwa na madalali wa kihalifu.
Recent Comments