Ajali mbaya ya Barabarani yatokea asubuhi hii mwenye barabara ya Mati road Sokoni Kithaga kata ya chaiakariga wilayani Tharaka South, pale gari aina ya Nissan 14 seater kutoka muungano wa uchukuzi KETNO ambayo ilikuwa inatoka sokoni Chiakariga kuelekea sokoni Kathwana Mwendo wa saa kumi asubuhi ya leo kubeba abiria ikipoteza mwelekeo na kubingiria mara kadhaa na kuanguka kwenye stesheni ya Mafuta ya petroli ya Total ndani sikoni Kithaga. Gari hio ambayo wakati wa kuanguka haikuwa na abiria ila Ndereva peke yake, Ndereva inasemekana amepata majeraha kiasi pale amapelekwa kwenye hosipitali ya kibinafsi ya Komarock modern hospital Kathwana. Imekuwa ni bahati gari hio haikugonga pump za mafuta katika stesheni hio ya Total jambo ambalo lingesababisha mlipuko wa poto, ila imeanguka hapo ndani na kuisha kabisa. Itakubukwa eneo hili la Kithaga barabara ya Marty road hupata ajali mara kwa mara ambalo ni eneo mwezi mmoja uliopita Father wa kanisa la kikatoliki la Marimanti Eliud Kinywa alipata ajali eneo hilo na kufariki.
Janzo cha ajali hio hakijabainika huku askari toka kituo cha polisi cha Chiakariga wakifika hapo kwa uchunguzi zaidi.

Recent Comments